Jumamosi, 28 Juni 2014

VUNJIKA MBAVU NA KING MAJUTO NDANI YA FILAMU YA INSIDE

Filamu hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na  BENY, pia utamuona marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.

Jumatatu, 13 Januari 2014

UZINDUZI WENYE WAIMBAJI ZAIDI YA 20 KUFANYIKA UBUNGO PLAZA HAPA BONGO. MESSY JACOB CHENGULA KUWEKA HISTORIA

Jamani kila kilicho cha Mungu kina thamani na kinaheshimika mbele ya wanadamu na mbele zake Mungu. Si kitu rahisi kichwa kimoja kukusanya waimbaji maarufu nchini Tanzania kuimba katika uzinduzi wa albamu moja yenye upako wa kipekee inayoenda kwa jina la la MUNGU WETU HABADIRIKI.

Mess Jacob Chengula ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania. Mungu amempa Neema ya kipekee sana katika huduma yake ya uimbaji. Nyimbo zake zimekubalika masikioni mwa Watanzania na wana Afrika Mashariki. Nyimbo hizi ukisikiliza hakika hutabaki kama ulivyokuwa kuwa. Ni lazima utoke katika hatua moja ya kiimani na kuingia katika hatua nyingine. Kwa sasa ni vigumu kuniamini kwasababu hujawahi kusikia na kama umewahi kusikia hukujua kuwa mtumishi wa Mungu Mess Jacob Chengula ndiye aliyeweza kuziimba hizi nyimbo.

Wa pili kutoka kulia ni Moss Jacom Chengula

Nisikuchoshe kwa maneno mengi, ngoja nikupeleke katika ratiba nzima ya uzinduzi huu.

ALBAMU: Mungu Habadiriki
ENEO: Ubungo Plaza jijini Dar es Salaama Tanzania

Eneo la tukio Ubungo Plaza

Ubungo Plaza ndani


MUDA: Saa 2:00 Asubuhi - 6:00 Mchana kutakuwa na Ibada ya kuweka wakfu albamu hii na kutakuwa na vinjwaji, chakula na keki.
Saa 6:00mchana na kuendelea tamasha la uzinduzi litaanza RASMI

TAREHE 02 . 03. 2013

MGENI RASMI: Naibu Waziri wa Mawasiliano Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh. Januari Makamba
KIINGILIO: VIP ni Tshs. 20,000
Viti Maalum ni Tshs. 10,000
Viti vya Kawaida ni Tshs. 5,000
Waimbaji
1. Rose Muhando
2. Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji)
3. Bahati Bukuku
4. Faraja Ntaboba (Congo)
5. Upendo Nkone
6. Stella Joel
7. Betrice Mwaipaja
8. Madam Ruti
9. Miriamu Lukindo
10. Edson Mwasabwite
11. Joshua Makondeko
12. Christina Matai
13. Ibrahimu Sanga
14. Maximilian Mwanamapinduzi
15. Kisa Blessing
16.Neema Gasper
17. Tumaini Njole
18. Silase Mbise
19. Victor Aron
20. Bony Mwaitege

Blogger: Rulea Sanga wa RumAfrica takuwepo kuchukua matukio siku hiyo.

MAWASILIANO
Simu; +255 (0) 752 880584 | +255 (0) 715 880 584
B/Pepe: messjacob5@gmail.com
Blogu: www.messchengula.blogspot.com
Facebook; Mess Jacom